TAARIFA KWA UMMA
OWM-TAMISEMI inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga
na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2015.Wanafunzi
waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali.
Jumla ya wanafunzi 55,003 wakiwemo wasichana 23,303 na wavulana31,700
wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi.Kati ya
wanafunzi waliochaguliwa 29,744 wakiwemo wasichana 11,450 nawavulana
18,294 sawa na asilimia 54.08 watajiunga na masomo ya Sayansina
Hisabati; na wanafunzi 25,259 wakiwemo wasichana 11,853 nawavulana
13,406 sawa na asilimia 45.92 wamechaguliwa kusoma masomoya Sanaa na
Biashara.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2015wataanza
muhula wa kwanza tarehe 18 Julai, 2015 na hakutakuwa nafursa ya
mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwakuripoti katika
shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunziatachelewa kuripoti kwa
zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya mwisho yakuripoti, nafasi yake
itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosanafasi.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano naVyuo
vya Ufundi mwaka 2015 inapatikana kwenye tovuti ya OWMTAMISEMI
ya www.pmoralg.go.tz
http://www.pmoralg.go.tz/noticeboard/tangazo-1040-20150630-Uchaguzi-wa-kujiunga-na-Kidato-cha-Tano-2015/
Imetolewa na Katibu Mkuu,
Home » Unlabelled » BOFYA HAPA KUPATA MATOKEO YA UCHAGUZI WA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO JULAI 2015.
Post a Comment