Baraza
la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya upimaji
wa darasa nne na kidato cha pili iliyofanyika Novemba 22 na 23 mwaka
jana, huku idadi kubwa ya wanafunzi wakifanya vyema katika mitihani
hiyo.
Akitangaza
matokeo hayo leo Jumatatu Januari 8, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk
Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 1,086,156 waliofanya mtihani
wa darasa la nne wamefaulu kati ya 1,158,444 waliofanya upimaji huo.
Amesema
wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata alama zenye madaraja ya A,B,C na D
wakati wanafunzi 72,288 sawa na asilimilia 6.24 wamepata alama za daraja
E, ambao ni ufaulu usioridhisha.
Kuhusu
matokea ya upimaji wa kidato cha pili, Dk Msonde amesema jumla ya
wanafunzi 433,453 sawa na asilimia 82.32 kati ya 486,742 waliosajiliwa
kufanya mtihani huo wamepata ujuzi wa maarifa ya kuwawezesha kuendelea
na kidato cha tatu.
Dk
Msonde alisema wanafunzi wa kidato cha pili 51,807 sawa na asilimia
10.68 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha
tatu.
Credit:mpekuzihuru
Post a Comment