Korea Kaskazini ilirusha kombora tarehe 29 Agosti 2017 kuelekea Bahari ya Japan, uongozi wa jeshi la Korea Kusini limebaini.
Korea Kaskazini ilifanya jaribio la kombora kuelekea bahari ya Japan,
askari wa Korea Kusini wamebaini. Kombora hilo lilipita kwenye anga ya
kaskazini mwa Japan, kwa mujibu wa serikali ya Japani, taarifa
iliyothibitishwa na Pentagon.
Jaribio hili linakuja wakati ambapo
mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Korea Kusini na Marekani
yanaendelea, mazoezi ambayo Korea Kaskazini inachukulia kama tishio la
moja kwa moja kwa usalama wake.
"Kombora lisilojulikana" lilirushwa
kutoka Sunan karibu na Pyongyang saa 5:57 saa za Korea Kaskazini (sawa
na saa siku ya Jumatatu saa 20:57 usiku saa za kimataifa), kwa mujibu wa
uongozi wa jeshi la Korea Kusini. "Korea Kusini na Marekani
wanatathmini kwa pamoja hali hiyo," uongozi wa jeshi la Korea Kusini
umeongeza. Kombora lililorushwa na Korea Kaskazini inaonekana kuwa
lilipita kwenye anga ya Japan, kwa mujibu wa shirika la habari la Kyodo.
Kwa mujibu wa NHK, kombora hilio lilipasuka vipande vitatu na
lilianguka katika pwani ya kisiwa cha Hokkaido.
Mfumo wa onyo wa mamlaka uliwashauri
wakazi wa eneo hilo kuchukua tahadhari, lakini kwa mujibu wa kituo cha
habari cha serikali ya Japan, hakuna hasara iliyotokea. Msemaji wa
Waziri Mkuu, Yoshihide Suga, amesema kuwa kombora hilo ni "tishio kubwa
kwa usalama" wa Japan.
Tukio hilo limechochea tahadhari ya
hatari ambayo watu walielekezwa kujificha katika maeneo yaliyo chini ya
ardhi ama kwenye majengo yaliyo imara.
Hakuna juhudi zilizofanywa na Japan
kulitengua kombora hilo lakini ilitoa onyo la kiusalama ikiwaambia raia
wake katika eneo la Hokkaido kujificha chini ya majumba yaliojengwa
ardhini.
Wakati huo huo Bwana Abe alisema kuwa
amezungumza na rais wa Marekani Donald Trump na kwamba wote
wamekubaliana kuiongezea shinikizo Korea Kaskazini.
Katika mfululizo wa majaribio yake ya
makombora ya hivi karibuni Korea kaskazini haijawahi kurusha makombora
yaliyopita juu ya ardhi ya nchi hiyo, hivyo tukio hili la sasa limeleta
wasiwasi mkubwa.
Credit by:RFI
Post a Comment