Akizungumza
na waandishi wa habari mkoani Arusha, Kamanda wa polisi, Liberatus
Sabas amesema kuwa majambazi waliouwawa watatu ni raia wa Kenya ambapo
bado majina yao kamili hayajajulikana huku raia wa Tanzania ametambulika
kwa jina la Sixtus Alfredy.
Kamanda
Sabas amesema kuwa ,polisi walianza kujibu majibizano hayo ndipo
walipofanikiwa kuua majambazi watatu ambao walikutwa na vitambulisho
vitatu vya Jamhuri ya Kenya vyenye majina ya Simon Githinji
Kariuki,Bonifas Mwanmgi Mbulu, Thadeo Kamau Njuguna na kitambulisho
kimoja cha UN-ICTR chenye jina la Chacha John Marwa.
Vitambulisho
vingine walivyokutwa navyo ni leseni ya udereva iliyotolewa Kenya yenye
jina la Thadeo Kamau Njuguna , kadi ya Benki ya Equity Master Card
yenye jina la Simon Githinji pamoja na kadi ya Benki ya Cooperative
yenye jina la Thadeo Kamau Njuguna , simu tano aina ya Nokia , Tecno na
Sumsung.
Amesema
kuwa, majambazi hao watatu kila mmoja alikutwa na bastola pamoja na
risasi , mabegi matatu meusi ambapo baada ya kuyafungua walikuta bunduki
aina ya AK 47 mbili, SMG moja, bastola tatu, magazine nne za SMG,
risasi 85 za SMG na AK 47 na risasi nyingine 28 za bastola.
Kamanda
Sabas amesema kuwa, tukio hilo lilitokea jana Septemba 17 mwaka huu
majira ya saa 3:30 usiku katika maeneo ya Chekereni wilayani Arumeru
ambapo polisi walipata taarifa za kiintelejensia toka Agosti 19 mwaka
huu juu ya kuwepo kwa kundi la majambazi wanaotoka nchi jirani ya Kenya
na kuja hapa nchini kwa nia ya kufanya uporaji kwa kushirikiana na
majambazi wenzao wa hapa nchini.
Alisema
miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika Hopsitali ya Mkoa ya Mount
Meru huku jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi zaidi wa kuwatafuta
watuhimiwa wengine waliotoroka katika tukio hilo na kubaini mtandao wa
majambazi hao.
Credit:Mpekuzi
Post a Comment