Taarifa
iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Shirika la Changamoto za
Milenia (MCC) linalomilikiwa na Serikali ya Marekani kwa ajili ya
kusaidia nchi zinazoendelea, ilieleza kuwa Bodi ya MCC ina matumaini
uchaguzi mkuu wa Tanzania utakaofanyika Oktoba 25 utakuwa huru na wa
haki, hasa ikizingatiwa umuhimu mkubwa ambao MCC inauweka katika haki za
kidemokrasia.
Kadhalika, taarifa hiyo imemkariri Balozi wa Marekani nchini, Childress akisema (Marekani) wanatambua rekodi ya Tanzania katika kukuza demokrasia na kwamba, wanaunga mkono na kusaidia jitihada endelevu za Tanzania katika kuimarisha taasisi zake za kidemokrasia.

“Tunatarajia kuona uchaguzi ulio huru, wa haki, wa amani na ambao utawasilisha matakwa ya watu wa Tanzania,” alisema Balozi Mark Childress.
Taarifa hiyo ya Marekani kuhusiana na uchaguzi mkuu nchini inatokana na mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi ya MCC iliyokutana juzi kujadili masuala mbalimbali yakiwamo ya utoaji wa misaada kwa Tanzania.
Taarifa hiyo ya Marekani kuhusiana na uchaguzi mkuu nchini inatokana na mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi ya MCC iliyokutana juzi kujadili masuala mbalimbali yakiwamo ya utoaji wa misaada kwa Tanzania.
Mbali
na Dk. Magufuli na Lowassa anayewakilisha pia muungano wa vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya NCCR-Mageuzi, NLD na
Chama cha Wananchi (CUF), wagombea wengine wa nafasi ya urais
wanaoendelea na kampeni kwa nia ya kumrithi Rais Jakaya Kikwete ni Fahmy
Dovutwa wa UPDP, Hashim Rungwe wa Chaumma, Anna Mghwira wa
ACT-Wazalendo, Chifu Lutasola Yemba wa ADC
Credit:Mpekuzi
Post a Comment