Mpaka
sasa Dk Magufuli ameshafanya kampeni katika mikoa ya Katavi, Rukwa,
Songwe, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Mtwara, Morogoro, Tanga, Mara na jana
alifikisha mkoa wa 11 Simiyu.
Kabla
ya kufika Mara na Simiyu, takwimu za CCM zilizotolewa na Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wazazi, Abdalah Bulembo, zimeonesha katika mikoa hiyo mingine
tisa, Dk Magufuli alikuwa ameshasafiri kwa barabara katika wilaya 42 na
kufanya mikutano 48 iliyo katika ratiba na mikutano mingine 260 isiyo
rasmi.
Moja
ya ajenda kubwa iliyombeba Dk Magufuli katika mikutano hiyo mpaka
Simiyu, ilikuwa uadilifu katika utendaji wake wa kazi katika wizara
mbalimbali alizofanya kazi katika miaka 20 ya utendaji wake, ikiwemo
katika Wizara ya Ujenzi, ambako ametumikia kwa miaka 15.
Uadilifu
Katika
mikoa mingi alikopita, uadilifu wake umezungumzwa kwa namna tatu
tofauti, ikiwemo mwenendo alioonesha katika nafasi yake ya Waziri katika
Wizara ya Ujenzi, iliyokuwa ya kipaumbele kibajeti.
Kwa
mfano katika Bajeti ya Serikali kwa mwaka huu wa fedha 2015/2016,
Wizara ya Ujenzi imekabidhiwa Sh trilioni 1.2 za wizara, huku Mfuko wa
Barabara ulio chini ya wizara hiyo, ukikabidhiwa zaidi ya Sh bilioni 866
na hivyo kwa ujumla kukabidhiwa Sh trilioni mbili, ambazo amepaswa
kuzisimamia.
Kwa
mujibu wa Dk Magufuli mwenyewe, akipiga hesabu ya fedha za umma
alizosimamia kwa ajili ya miradi ya ujenzi wa barabara katika miaka kumi
ya uongozi wake, ni zaidi ya Sh trilioni 9.5, lakini hakula hata senti
tano, badala yake akajenga mtandao mrefu wa barabara za lami nchi nzima.
Namna
ya pili ya kuzungumzia uadilifu wake ni ushirikiano wake na watendaji
na wadau wa sekta ya ujenzi, ambao amekuwa akiwapa kazi za mabilioni ya
shilingi, katika kuwatumikia Watanzania.
Namna
ya tatu iliyotumika kuelezea uadilifu wa Dk Magufuli, imeelezwa na Jaji
Joseph Warioba mkoani Mara, ambapo alisema mwaka 1996, aliteuliwa na
Rais Benjamini Mkapa, kuongoza Tume ya Kero za Rushwa.
Katika
uchunguzi wao, Jaji Warioba alisema walibaini rushwa kubwa na nyingi
zilikuwa katika sekta ya ujenzi wa barabara, lakini akafafanua baada ya
Dk Magufuli kuanza kufanya kazi katika sekta hiyo, kelele ya rushwa
katika sekta hiyo imetoweka.
Uchapakazi
Mbali
na uadilifu, ajenda nyingine iliyombeba Dk Magufuli na kusababisha awe
kivutio kikubwa kwa maelfu kwa maelfu ya wananchi waliojitokeza katika
mikutano yake, ni sifa ya uchapakazi wake ambayo imeendana na matokeo
yanayoonekana ya kazi hiyo.
Mbali
na watumishi, ukali wake pia umejidhihirisha mara kwa mara
alipozungumzia Baraza la Mawaziri atakalounda na hasa Waziri wa Ujenzi,
akisema huyo waziri atakayemteua, kama hawezi kazi aseme mwenyewe kabla
ya kutimuliwa, kauli ambayo pia imepokewa kwa shangwe na wananchi.
Ubora jukwaani
Dk
Magufuli pia katika mikoa hiyo 11, ameonesha umahiri mkubwa wa kutawala
majukwaa kwa mbinu mbalimbali, ikiwemo uwezo wa kutoa salamu na vionjo
vya makabila zaidi ya kumi jambo lililokuwa likiwavutia wananchi wengi
katika mikutano ambayo imekuwa ikifikia mpaka 15 kwa siku.
Akifafanua
sababu ya kutumia lugha za makabila mbalimbali, Dk Magufuli amekuwa
akisema mwitikio wa salamu hizo, umekuwa ukionesha namna jamii ya
Tanzania ilivyo na umoja kwa makabila mbalimbali kukutana katika
mikutano yake na kufurahia pamoja.
Mara
kadhaa baada ya kutoa salamu hizo, alikuwa akimalizia kwa kusema hiyo
ndio Tanzania yenye kila mchanganyiko wa kabila, lakini wanaishi kwa
umoja na amani bila aina yoyote ya ubaguzi.
Baada
ya kutoa salamu hizo, Dk Magufuli pia amekuwa akiomba kura kutoka kwa
vyama vyote, kuanzia CCM, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi, ACT na kwa watu
wasio na vyama, huku akiwaambia kuwa kazi yake itakuwa kuwaletea
maendeleo na kwa kuwa maendeleo hayabagui, ndio maana anaomba kura za
vyama vyote.
Ahadi zake
Dk
Magufuli katika mikutano hiyo, amekuwa akiahidi kushusha bei ya vifaa
vya ujenzi hasa saruji, mabati na misumari, ili wananchi wanaofanya kazi
wajenge nyumba bora.
Katika
kuongeza idadi ya Watanzania wanaofanya kazi ili kufikia lengo hilo, Dk
Magufuli alisema katika kila mtaa na kijiji, Serikali yake itatoa Sh
milioni 50 kwa ajili ya kuanzisha na kukuza biashara ndogo za wanawake
na vijana.
Alisema
atataka kila anayefanya kazi apate kipato kizuri kitakachomsaidia
kukabiliana na mahitaji ya maisha yake, ikiwemo kujenga nyumba bora
kutokana na kushushwa kwa bei za bidhaa za ujenzi.
Credit:Mpekuzi
Post a Comment