Dk
Magufuli aliwaambia wakazi wa kijiji cha Mlangali wilayani Ludewa kuwa
serikali za awamu nne zilizopita zilifanya makubwa kwa kuboresha
mazingira ya maendeleo hivyo awamu yake itakuwa ni ya kukamilisha
mabadiliko.
"Awamu
ya kwanza ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere ndiyo iliyoleta Uhuru kutoka
kwa wakoloni na ukombozi wa kweli kwa kuunganisha makabila zaidi ya
121.
"Awamu
za Mzee Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Kikwete hizi
nazo zimefanya makubwa kwa kuendelea kutuweka pamoja kwa amani bila
kupigana na kujenga barabara kama hizi japo za vumbi lakini zinapitika, "
alisema Dk Magufuli.
Alisema
kutokana na mafanikio ya Serikali zilizopita, awamu ya tano itakuwa ni
ya maendeleo ya barabara, umeme, viwanda, elimu, maji, afya, ajira na
kuboresha mazingira ya wafanyakazi na wakulima.
Kauli
ya mgombea huyo inakuja siku moja baada ya mgombea wa Urais wa Chadema
kupitia mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa
kuahidi juzi kuwa iwapo atapitishwa, Serikali yake itakuwa ni ya
mabadiliko na ukombozi.
Dk Magufuli alisema atakuwa rais wa Watanzania wa dini na vyama vyote.
credited:Mpekuzi
Post a Comment