Bw.Makene
ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa baraza la vijana la vyama
vinavyounda UKAWA na waandishi wa habari ambao pia viongozi hao
wametumia nafasi hiyo kuiomba tume ya uchaguzi kuwakemea viongozi na
watendaji wa serikali kufanya kazi za siasa kwa lengo la kukibeba chama
tawala.
Viongozi
hao wa vijana wamesema hatua ya viongozi na watendaji wa serikali ya
kujihusisha moja kwa moja na kampeni za CCM huku wengine wakitumia
rasilimali za umma na vyombo vya dola kukandamiza vyama vya upinzani
inathibitisha ukweli wa malalamiko yao.
(credit: mpekuzi.)
Post a Comment