Wanaharakati nchini Syria wanasema
kuwa mlipuko kwenye msikiti mmoja katika mkoa ulio kaskazini magharibi
wa Idlib umewaua takriban wanachama 25 wa kundi lenye uhusiano na kundi
la Al-Qaeda la Al Nusra Front.
Shirika la haki za binadamu lenye
makao yeke nchini Uingereza linasema kuwa mlipuko huo kwenye mji wa
Ariha ulitokea wakati wanachama wa kundi hilo walipokutana kupata
chakula.Haijabainika ni nani aliendesha shambulizi hilo.
Mapema ndege za kivita za Syria zilishambulia waasi karibu na mji wa Aleppo kuzima jaribio ya kutaka kuuteka mji huo.
Utawala nchini Syria unasema kuwa takriban wanamgambo 100 waliuawa.
credited by BBC
Post a Comment