Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiteremka kwenye ndege.
Ndege
iliyombeba Mhe. Magufuli na Mhe. Samia kutoka Dodoma wakati ikiwasili
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Makada na wanachama wa CCM wakijiandaa kuwapokea viongozi hao.
Magufuli akizungumza na wanachama pamoja na wananchi (hawapo pichani) waliojitokeza kumlaki uwanjani hapo.
Wanachama wa chama hicho waliojitokeza kumsikiliza kwenye Uwanja wa Zakheem, Mbagala jijini Dar.
Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda hawakuwa nyuma katika shamrashamra hizo.
MGOMBEA wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe.
Dk. John Pombe Joseph Magufuli, leo ametambulishwa rasmi kwa wakazi wa
Jiji la Dar, ambapo amepokelewa kwa kishindo na makada wa chama hicho
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kuelekea
Mbagala - Zakheem ambako alizungumza na wakazi wa jiji la Dar.
(Habari / Picha: Brighton Masalu / GPL)
Post a Comment