Hukumu
hiyo ilitolewa leo na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Aishiel Sumari
baada ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali,
Tamari Mndeme kukubali rufaa hiyo.
Mbali
na sababu za rufaa zilizowasilishwa mahakamani na wakili wa Mbowe,
Peter Kibatala, wakili Mndeme aliiongeza sababu zingine mbili
zinaonyesha mapungufu ya hukumu hiyo.
Wakili
Mndeme alimweleza Jaji kuwa shitaka lenyewe na maelezo ya shitaka
vilikuwa vinatofautiana hivyo kuathiri uhalali wa shitaka na uhalali wa
hukumu iliyomtia hatiani Mbowe.
Mbowe
alitozwa faini ya Sh1 milioni au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela
kwa kosa la kumshambulia mwangalizi wa ndani wa uchaguzi mkuu wa 2010
katika wilaya ya Hai, Nassir Yamin.
Hukumu
hiyo iliyolalamikiwa na Mbowe kuwa haikumtendea haki kwani kesi hiyo
ilifunguliwa kisiasa, ilitolewa Juni 17 mwaka huu na Hakimu Mkazi wa
wilaya ya Hai wakati huo, Denis Mpelembwa.
Hata
hivyo, Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), na mgombea ubunge wa Jimbo la Hai alilipa faini hiyo
na kuachiwa huru na Mahakama ya wilaya ya Hai.
Credit:Mpekuzi
Post a Comment