Mwandishi wa Habari kutoka The Guardian, Ndeninsia Lisley (kushoto) akionesha kadi yake ya matibabu kwa wanahabari.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF,
Athuman Rehan (kulia) akimkabidhi kadi ya matibabu, Ndeninsia
anayeshudia katikati ni mwenyekiti wa kampeni ya Media Car Wash,
Benjamin Thompson.(P.T)
Denis Mtima wa Global Publishers
(kushoto) akikabidhiwa kadi yake kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na
Utafiti wa NHIF, Athuman Rehan (kulia).
Baadhi ya wanakamati ya Harambee ya Media Car Wash wakiwa kwenye mkutano huo.
Kutoka kushoto , Benjamin Thompson,
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF, Athuman Rehan (katikati)
pamoja na Ofisa utekelezaji wa Mfoko wa NHIF, Hance Mwankenya.
Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo.
Ofisa utekelezaji wa mfoko wa Bima ya Afya kutoka NHIF, Hance Mwankenya (kulia) akizungumza jambo kwenye mkutano huo.
MFOKO wa
Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) leo umekabidhi kadi za matibabu kwa baadhi
ya wanahabari waliojisajili katika Kampeni ya Media Car Washi
inayoendelea hapa nchini kupitia kwa mwenyekiti wa kampeni hiyo,
Benjamin Thompson.
Akizungumza
leo katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Msimbazi Center jijini
Dar es Salaam kwenye kikundi cha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali
vya habari, Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Athuman Rehan amesema kuwa
anapongeza kampeni hiyo ya ‘Media Car Wash’ iliyoanzishwa kwa ajili ya
kusaidiana katika mambo mbalimbali hususani ya kiafya.
Amesema
kuwa zoezi la wanahabari kujiunga katika mfumo wa bima ya afya ni
mojawapo ya mafanikio katika kutatua changamoto ambazo zingeweza
kuwakabili wanahabari wakati wa kutafuta matibabu kwa kulipia pesa
taslimu.
Alisema
kuwa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ni Shirika la Umma lililoanzishwa
kwa sheria namba 8 ya mwaka 1999 ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa lengo la kuweka utaratibu wa upatiakanaji wa huduma za afya
nchini kwa njia rahisi na kwa uchangiaji nafuu.
Aidha,
aliongeza kuwa mfuko wa NHIF umekwisha anzisha mpango mpya unaoitwa
‘Kikoa’ ambao lengo lake ni kutoa huduma za afya kwa kadi ama vikundi
ambavyo watu wake wameajiriwa na hupata kipato chao kwa msimu kama vile
kikundi cha saccos, vibindo, vikoba, na hata umoja wa watu wa bodaboda.
Vilevile
katika mfuko huo mwanachama atakayetakiwa kuwa ameunganishwa kwenye
mfuko huo ni, mke, watoto walio chini ya miaka 18 pamoja na wazazi
wawili kupitia kampeni hiyo, ambapo mwanachama mmoja atatakiwa kulipia
kiasi cha shilingi 76,800/= na kujipatia matibabu kwa muda wa mwaka
mzima, michango hiyo ikipitia kwenye uongozi wa vikundi na kuwasilisha
NHIF ili vitambulisho vianze kutolewa mara moja.
Kampeni
hiyo ya Media Car Wash bado inaendelea kwa mikoa mingine ili kuendeleza
mchakakato wa kufikia lengo kuu, wanahabari Kanda ya Ziwa kwa
kushirikiana na wenzao wa Jijini Dar es Salaam, Agosti 15 mwaka huu,
wataosha magari kwenye viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza.
PICHA /HABARI: DENIS MTIMA NA DEOGRATIUS MONGELA/GPL
Post a Comment