Watu waliokuwa na bunduki wamemuuwa mkuu wa usalama wa zamani wa Burundi na mshauri mkubwa wa Rais Pierre Nkurunziza.
Walioshuhudia
tukio hilo wanasema Jeneral Adolphe Nshimirimana alikufa pale gari lake
liliposhambuliwa katika mji mkuu, Bujumbura.
Umoja wa Ulaya umesema mauaji yake yamezidisha wasiwasi, na kwamba juhudi za upatanishi lazima zianze tena.
Burundi imepita katika miezi kadha ya ghasia baada ya Rais Nkurunziza kuania na kushinda muhula wa tatu wa uongozi.
Inafikiriwa
kuwa Jenerali Nshimirimana bado alikuwa na mchango mkubwa katika
usalama, hata baada ya kutolewa kuwa mkuu wa usalama nchini Burundi.
Muandishi wa habari wa Ufaransa ambaye alipiga picha za pahala jenerali huyo aliposhambuliwa, alikamatwa na kupigwa.BBC
Post a Comment