Taarifa Rasmi ya serikali Ya Tanzania juu ya Ajali katika Msikiti wa Makkah - Saudi Arabia, Mahujaji wa Watanzania wote wako Salama.

Msanii King Majuto akiwa na Mahujaji wenzake wakiwa salama salimini baada ya ajali hiyo
  ***
Kufuatia mvua  ilioambatana na upepo mkali na kusababisha kuanguka kwa mashine ya ujenzi wa upanuzi wa eneo la Tawaf ulipo msikiti wa Makkah, msikiti huo umeanguka na kusababisha vifo vya mahujaji.  

Kwa mujibu wa Televisheni ya Saudi Arabia, Saudi TV hadi sasa watu 107 wamefariki dunia na wengine takriban 200 wamejeruhiwa. 
 
Kufuatia ajali hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kupitia Ofisi za Ubalozi Riyadh unathibitihsa kuwa Mahujaji wa Tanzania wameanza kuwasili Jeddah kuelekea Makkah leo tarehe 12 Septemba 2015 wakitokea Madina. 

Hadi sasa Wizara haijapokea taarifa ya Watanzania waliopoteza maisha wala kujeruhiwa kwenye ajali hiyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
12 Septemba, 2015
Mmoja wa viongozi wa Mahujaji wa Tanzania akiongea katika kikao cha dharura na mahujaji hao baada ya krini la ujenzi na katika eneo la Tawaf ulipo msikiti wa Makkah kuanguka  na kusababisha vifo vya mahujaji 107 na majeruhi zaidi ya 200. Hakuna Mahujaji wa Tanzania walioathirika katika ajali hiyo.
Baadhi ya Mahujaji wa Tanzania wakiwa Makkah salama salimini baada ya ajali hiyo

Credit:Mpekuzi

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright Enter Media Published.. Blogger Templates
Back To Top