Barua
ya Jeshi la Polisi ambayo imetolewa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Z.Msangi ikikataza
maandamano hayo na kukubali kufanyika kwa mkutano tu iko hapo chini.
Tangazo kwa umma.
Mnamo
tarehe 10/08/2015 ofisi ya mkuu wa polisi wilaya ya mbeya ilipokea
barua toka chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) inayohusu taarifa
ya mkutano wa hadhara utakaofanyika tarehe 14/08/2015 katika viwanja
vya ruanda nzovwe.lengo la mkutano huo ni mgombea wa raisi kuomba
wadhamini
Leo
tarehe 13/08/2015 jeshi la polisi mkoa wa mbeya lilikutana na uongozi
wa chama cha demokrasia na maendeleo akiwemo mbunge wa mbeya mjini na
baadhi ya madiwani katika eneo la usalama wa chama hicho katika ofisi ya
kamanda wa polisi mkoa wa mbeya na kufanya mazungumzo kisha kufikia
makubaliano kama walivyotoa taarifa yao kuwa hakutakuwa na maandamano
bali ni mkutano. Hii inatokana na;
- Sababu za kiusalama
- Kutozuia watumiaji wengine wa barabara hiyo ikizingatiwa barabara kuu itakayotumika ni moja.
Hivyo
basi kamanda wa polisi mkoa wa mbeya anatoa rai kwa wananchi kutofanya
au kulazimisha maandamano yoyote yawe ya miguu au pikipiki.hii ieleweke
kwamba si maandamano bali ni mkutano wa hadhara utakaofanyika katika
viwanja hivyo. Kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
(credited by mpekuzi huru).
Post a Comment